Bikira Ona pia Maria, Mama wa Yesu Mwanamume au mwanamke wa umri wa kuweza kuolewa ambaye kamwe hajapata kujamiiana. Katika maandiko, bikira anaweza kumwakilisha mtu ambaye ni msafi kimaadili (Ufu. 14:4). Bikira atachukuwa mimba na atazaa mwana, Isa. 7:14 (Mt. 1:23; 2 Ne. 17:14). Ufalme wa mbinguni unafananishwa na wanawali kumi, Mt. 25:1–13. Katika mji wa Nazarethi nilimwona bikira, ambaye alikuwa mama wa Mwana wa Mungu, 1 Ne. 11:13–18. Maria alikuwa bikira, chombo cha thamani na kilichochaguliwa, Alma 7:10.