Mtakatifu Ona pia Kanisa la Yesu Kristo; Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Wakristo Muumini mwaminifu wa Kanisa la Yesu Kristo. Nikusanyieni pamoja Watakatifu wangu, Zab. 50:5. Sauli alifanya mengi maovu kwa Watakatifu huko Yerusalemu, Mdo. 9:1–21. Petro pia akawatelemkia Watakatifu waliokuwa wakikaa Lida, Mdo. 9:32. Neema na amani kwa wote waliokaa Rumi, walioitwa kuwa Watakatifu, Rum. 1:7. Ninyi ni raia wenyeji pamoja na Watakatifu, Efe. 2:19–21. Nililiona Kanisa la Mwanakondoo, ambao walikuwa Watakatifu wa Mungu, 1 Ne. 14:12. Mtu wa asili ni adui kwa Mungu isipokuwa amekuwa mtakatifu kwa njia ya upatanisho wa Kristo, Mos. 3:19. Mimi, Bwana, nimeibariki nchi kwa ajili ya matumizi ya Watakatifu wangu, M&M 61:17. Shetani hufanya vita na Watakatifu wa Mungu, M&M 76:28–29. Fanya kazi kwa bidii kwa kuwatayarisha Watakatifu kwa ajili ya hukumu ambayo inakuja, M&M 88:84–85. Watakatifu yawapasa kutoa mali zao kwa maskini na walioteseka, M&M 105:3. Ofisi zilizoko hapo juu nimezitoa kwa ajili ya kazi ya huduma na ya kuwakamilisha Watakatifu wangu, M&M 124:143 (Efe. 4:12).