Mwanakondoo wa Mungu Ona pia Lipia dhambi, Upatanisho; Pasaka; Yesu Kristo Jina la Mkombozi ambalo linamwelezea Yesu kama dhabihu iliyotolewa kwa niaba yetu. Aliletwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni, Isa. 53:7 (Mos. 14:7). Tazama mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu, Yn. 1:29 (Alma 7:14). Ninyi mlikombolewa kwa damu ya thamani ya Kristo, kama ya mwanakondoo asiye na ila, 1 Pet. 1:18–20. Astahili Mwanakondoo aliyechinjwa, Ufu. 5:12. Tunamshinda Shetani kwa damu ya Mwanakondoo, Ufu. 12:11. Hawa wamefanywa kuwa weupe kwa damu ya Mwanakondoo, kwa sababu ya imani yao katika yeye, 1 Ne. 12:11. Mwanakondoo wa Mungu ndiye Mwana wa Baba wa milele, na Mwokozi wa ulimwengu, 1 Ne. 13:40 (1 Ne. 11:21). Lieni kwa Baba kwa nguvu katika jina la Yesu, ili pengine mpate kuoshwa kwa damu ya Mwanakondoo, Morm. 9:6 (Ufu. 7:14; Alma 34:36). Mwana wa Mtu ndiye Mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, Musa 7:47.