Etheri
Nabii wa mwisho wa Wayaredi katika kitabu cha Mormoni (Eth. 12:1–2).
Kitabu cha Etheri
Kitabu katika Kitabu cha Mormoni ambacho kina sehemu za kumbukumbu ya Wayaredi. Wayaredi walikuwa ni kikundi cha watu walioishi katika dunia ya magharibi karne nyingi zilizopita kabla ya watu wa Lehi. Kitabu cha Etheri kilichukuliwa kutoka katika mabamba ishirini na manne yaliyogunduliwa na watu wa Limhi (Mos. 8:8–9).
Mlango wa 1–2 inaeleza namna Wayaredi walivyoacha nyumba zao wakati wa Mnara wa Babeli na kuanza safari yao kwenda mahali ambako sasa kunajulikana kama bara la Marekani. Mlango wa 3–6 inaeleza kwamba kaka wa Yaredi alimwona Mwokozi kabla hajazaliwa na kwamba Wayaredi walisafiri katika boti nane. Mlango wa 7–11 inaendeleza historia ya uovu ambao ulitawala kiasi kikubwa cha historia ya Wayaredi. Moroni ambaye alihariri kumbukumbu ya Etheri, aliandika katika mlango wa 12–13 juu ya maajabu yaliyofanywa kwa imani na juu ya Kristo na Yerusalemu Mpya ijayo. Mlango wa 14–15 inaelezea jinsi Wayaredi walivyokuja kuwa taifa lenye nguvu lakini likaangamizwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya uovu.