Mama Ona pia Familia; Hawa; Wazazi Jina takatifu kwa mwanamke mwenye kuzaa au kupanga watoto. Akinamama husaidia katika mpango wa Mungu kwa kutoa miili yenye kufa kwa ajili ya watoto wa kiroho wa Mungu. Adamu alimwita mke wake jina la Hawa, kwa sababu yeye alikuwa mama wa wote walio hai, Mwa. 3:20 (Musa 4:26). Waheshimu baba na mama yako, Ku. 20:12 (Efe. 6:1–3; Mos. 13:20). Usiache sheria ya mama yako, Mit. 1:8. Mpumbavu humdharau mama yake, Mit. 15:20 (Mit. 10:1). Usimdharau mama yako akiwa mzee, Mit. 23:22. Watoto wake na mumewe huinuka na kumwita heri na mumewe naye humsifia, Mit. 31:28. Mama wa Yesu alisimama pembeni ya msalaba, Yn. 19:25–27. Askari elfu mbili wa Walamani walifundishwa na mama zao, Alma 56:47 (Alma 57:21). Mama yetu mtukufu Hawa alikuwa ni miongoni mwa wale maarufu na wakuu ambao Bwana aliwafundisha katika ulimwengu wa roho, M&M 138:38–39.