Hofu yaweza kuwa na maana mbili: (1) hofu juu ya Mungu ni kujisikia uchaji na heshima Kwake na kutii amri Zake; (2) kumhofia mtu, hatari za kimwili, maumivu, na uovu ni kuwa na woga na mambo ya jinsi hiyo na kuyaogopa sana.
Manabii waliwachochea watu daima ili kuwaweka katika hofu ya Bwana, Eno. 1:23 .
Alma na wana wa Mosia walianguka chini, kwani hofu ya Bwana ilikuja juu yao, Alma 36:7 .
Timizeni wokovu wenu kwa hofu na kutetemeka, Morm. 9:27 .
Wao wasio kuwa na hofu na mimi, nitawasumbua na kuwafanya watetemeke, M&M 10:56 .
Yule mwenye hofu na mimi atazitazamia ishara za kuja kwa Mwana wa Mtu, M&M 45:39 .
Usingemwogopa mwanadamu zaidi kuliko Mungu, M&M 3:7 (M&M 30:1, 11 ; 122:9 ).
Usihofu kutenda mema, M&M 6:33 .
Yeyote aliye mali ya kanisa langu hahitaji kuogopa, M&M 10:55 .
Kama mmejiandaa, hamtaogopa, M&M 38:30 .
Jivueni wenyewe katika hofu, M&M 67:10 .
Furahini, na msiogope, kwani Mimi Bwana niko pamoja nanyi, M&M 68:6 .
Msiwaogope maadui zenu, M&M 136:17 .