Uzima wa Milele Ona pia Kuinuliwa; Lipia dhambi, Upatanisho; Taji; Utukufu wa Selestia; Uzima Kuishi milele kama familia katika uwepo wa Mungu (M&M 132:19–20, 24, 55). Uzima wa milele ndiyo tuzo kuu zaidi ya Mungu kwa mwanadamu. Wewe unayo maneno ya uzima wa milele, Yn. 6:68. Uzima wa milele ndiyo huu, kwamba wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo, Yn. 17:3 (M&M 132:24). Piga vita vile vizuri vya imani, shika uzima ule wa milele, 1 Tim. 6:12. Watu wako huru kuchagua uhuru na uzima wa milele, 2 Ne. 2:27 (Hel. 14:31). Kujali mambo ya kiroho ndiyo uzima wa milele, 2 Ne. 9:39. Ndipo ninyi mtakuwa katika ile njia nyembamba ile iongozayo katika uzima wa milele, 2 Ne. 31:17–20. Kuamini katika Kristo na kustahimili hadi mwisho ndiyo uzima wa milele, 2 Ne. 33:4 (3 Ne. 15:9). Yeye aliye na uzima wa milele ndiye tajiri, M&M 6:7 (M&M 11:7). Uzima wa milele ndiyo zawadi ya Mungu iliyo kuu kupita zote, M&M 14:7 (Rum. 6:23). Wenye haki watapokea amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao, M&M 59:23. Wale wastahimilio hadi mwisho watavikwa taji la uzima wa milele, M&M 66:12 (M&M 75:5). Wote wanaokufa pasipo injili ambao wangeipokea kama wangeliishi ni warithi wa ufalme wa selestia, M&M 137:7–9. Kazi na utukufu wa Mungu ni kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu, Musa 1:39. Mungu hutoa uzima wa milele kwa walio watiifu, Musa 5:11.