Alma Mzee Nabii Mnefi aliye katika Kitabu cha Mormoni ambaye alilianzisha kanisa katika siku za Mfalme mwovu Nuhu. Alikuwa kuhani wa Mfalme mwovu Nuhu na wa uzao wa Nefi, Mos. 17:1–2. Baada ya kumsikiliza na kumwamini Abinadi aliondolewa na mfalme. Alitoroka, akajificha, na aliyaandika maneno ya Abinadi, Mos. 17:3–4. Alitubu na kuyafundisha maneno ya Abinadi, Mos. 18:1. Alibatiza katika maji ya Mormoni, Mos. 18:12–16. Alianzisha kanisa, Mos. 18:17–29. Alifika Zarahemla pamoja na watu wake, Mos. 24:25. Alipewa mamlaka juu ya kanisa, Mos. 26:8. Alihukumu na kuliongoza Kanisa, Mos. 26:34–39. Alimpatia mwanawe ofisi ya ukuhani mkuu, Alma 4:4 (Mos. 29:42; Alma 5:3).