Sikiliza Ona pia Mtiifu, Tii, Utii; Sikio Kusikia na kutii sauti au mafundisho ya Bwana. Bwana atamwinua nabii kama Musa, na watu wanapaswa kumsikiliza yeye, Kum. 18:15. Kusikia ni bora kuliko mafuta ya beberu wa dhabihu, 1 Sam. 15:20–23. Hatukuwasikiliza watumishi wa Bwana, manabii, Dan. 9:6. Watu wenye haki wasikilizao maneno ya manabii hawataangamia, 2 Ne. 26:8. Kama hamtasikia sauti ya mchungaji mwema, ninyi si kondoo wake, Alma 5:38 (Hel. 7:18). Sikilizeni, Enyi watu wa kanisa langu, M&M 1:1. Wale waisikilizao sauti ya Roho huangazwa na kuja kwa Baba, M&M 84:46–47. Wao walikuwa wavivu kuisikiliza sauti ya Bwana; kwa hiyo, naye amekuwa mzito kuzisikiliza sala zao, M&M 101:7–9. Wale ambao hawasikii amri huwarudi, M&M 103:4 (Musa 4:4).