Nyama Ona pia Hali ya Kufa, enye Kufa; Mwanadamu wa Tabia ya Asili; Mwili; Tamaa za kimwili Nyama ina maana nyingi: (1) mkusanyiko wa seli ndogo laini ambazo hutengeneza miili ya wanadamu, wanyama, ndege, au samaki; (2) wenye kufa; au (3) maumbile au tamaa za mwanadamu wa asili. Mkusanyiko wa seli za mwili Wanyama watakuwa chakula chenu, Mwa. 9:3. Wanyama wasiuawe bila sababu, TJS, Mwa. 9:10–11 (M&M 49:21). Wanyama na ndege ni kwa ajili ya chakula na mavazi ya mwanadamu, M&M 49:18–19 (M&M 59:16–20). Yatupasa kula nyama kwa kiasi, M&M 89:12–15. Mwili wenye kufa Yesu ndiye Mwana pekee wa Baba katika mwili wenye kufa, Yn. 1:14 (Mos. 15:1–3). Adamu akawa mwenye mwili wa kwanza, Musa 3:7. Tamaa ya asili ya mwanadamu Amelaaniwa mwanadamu aufanyaye mwili kuwa mkono wake, Yer. 17:5. Roho iradhi, bali mwili ni dhaifu, Mk. 14:38. Tamaa ya mwili haitokani na Baba, 1 Yoh. 2:16. Nefi alihuzunika kwa sababu ya mwili wake na dhambi zake, 2 Ne. 4:17–18, 34. Msijipatanishe wenyewe kwa ibilisi wala mwili, 2 Ne. 10:24.