Shamba la mizabibu la Bwana Ona pia Israeli; Shamba Ishara ya shamba la kazi za kiroho. Katika maandiko shamba la mizabibu la Bwana kwa kawaida humaanisha nyumba ya Israeli au ufalme wa Mungu duniani. Wakati mwingine humaanisha watu wa ulimwengu kwa ujumla. Shamba la mizabibu la Bwana wa Majeshi ni nyumba ya Israeli, Isa. 5:7 (2 Ne. 15:7). Yesu alitoa mfano wa watumishi katika shamba la mizabibu, Mt. 20:1–16. Israeli ni kama mzeituni uliotunzwa katika shamba la mizabibu la Bwana, Yak. (KM) 5. Watumishi wa Bwana watapogoa shamba lake la mizabibu kwa mara ya mwisho, Yak. (KM) 6. Bwana atawabariki wote ambao wanatumika katika shamba la mizabibu, M&M 21:9 (Alma 28:14). Tumikeni ninyi katika shamba langu la mizabibu kwa mara ya mwisho, M&M 43:28.