Kugeuka sura
Hali ya watu ambao kwa muda wanageuka katika sura na hali ya asili—ambako ni, kuinuliwa kwa kiwango cha juu zaidi kiroho—ili kwamba waweze kustahmili uwepo na utukufu wa viumbe wa mbinguni.
Kugeuka sura kwa Kristo
Petro, Yakobo, na Yohana walimwona Bwana akitukuzwa na kugeuka sura mbele yao. Kabla yake Mwokozi alikuwa amemwahidi Petro kwamba angepokea funguo za ufalme wa mbinguni (Mt. 16:13–19; 17:1–9; Mk. 9:2–10; Lk. 9:28–36; 2 Pet. 1:16–18). Katika tukio hili muhimu, Mwokozi, Musa, na Elia (Eliya) walitoa funguo za ukuhani ambazo ziliahidiwa kwa Petro, Yakobo, na Yohana. Kwa funguo hizi za ukuhani, Mitume walikuwa na uwezo wa kuendeleza kazi ya ufalme baada ya Kupaa kwa Yesu.
Joseph Smith alifundisha kwamba juu ya ule Mlima wa Kugeuka sura, Petro, Yakobo, na Yohana pia waligeuka sura. Waliona ono la dunia kama itakavyoonekana katika hali yake ya baadaye ya kutukuzwa (M&M 63:20–21). Waliwaona Musa na Eliya, viumbe wawili waliobadilishwa, na walisikia sauti ya Baba. Baba alisema, “Huyu ndiye Mwanangu Mpendwa wangu ninayependezwa sana naye; msikilizeni yeye” (Mt. 17:5).