Sio mcha mungu Ona pia Chafu, Uchafu; Dhambi; Kutokuwa Adilifu, Siyo Adilifu; Ovu, Uovu Mtu fulani au jambo fulani ambalo halilingani na mapenzi au amri za Mungu; mwovu na asiye mtakatifu. Njia ya asiye mchamungu itapotea, Zab. 1:6. Kama mwenye haki ataokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu ataonekana wapi, 1Â Pet. 4:18. Mjikane wenyewe kutomcha Mungu kwenu kote, Moro. 10:32. Kisasi chaja upesi juu ya wasiomcha Mungu, M&M 97:22. Mwokozi hakupaza sauti yake miongoni mwa wasio mcha Mungu, M&M 138:20.