Mjane Ona pia Ustawi Mwanamke ambaye mume wake amefariki na hajaolewa tena. Yatima na mjane watakuja na watakula, Kum. 14:29. Huyu mjane maskini ametia vyote alivyokuwa navyo, Mk. 12:41–44. Kuwatembelea yatima na wajane katika dhiki yao, Yak. (Bib.) 1:27. Bwana atakuwa shahidi mwepesi dhidi ya wale ambao huwanyanyasa wajane, 3 Ne. 24:5 (Zek. 7:10). Wajane na mayatima watatunzwa kwa mali hiyo, M&M 83:6 (M&M 136:8).