Alichagua, Chagua, Chaguliwa (kitenzi) Ona pia Haki ya uamuzi; Huru, Uhuru; Ita, Itwa na Mungu, Wito Bwana ateuapo, au kuchagua, mtu au kikundi, kwa kawaida pia Yeye huwaita kutumikia. Chagueni hivi leo mtakayemtumikia, Yos. 24:15 (Alma 30:8; Musa 6:33). Nimekuchagua katika tanuru ya mateso, Isa. 48:10 (1 Ne. 20:10). Waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache, Mt. 22:14 (Mt. 20:16; M&M 95:5; 121:34, 40). Si ninyi mlio nichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, Yn. 15:16. Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima, 1 Kor. 1:27. Alituchagua sisi kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, Efe. 1:4. Tuko huru kuchagua uhuru na uzima wa milele au utumwa na mauti, 2 Ne. 2:27. Watu mashuhuri na walio wakuu walichaguliwa toka mwanzo, M&M 138:55–56. Israeli alichaguliwa na Mungu, Musa 1:26. Ibrahimu alichaguliwa kabla hajazaliwa, Ibr. 3:23.