Roma Ona pia Ufalme wa Kirumi Katika Agano Jipya, ni mji mkuu wa Ufalme wa Kirumi, ulioko juu ya Mto Tiberi katika Italia (Mdo. 18:2; 19:21; 23:11). Paulo alifundisha injili katika Roma wakati alipokuwa mfungwa wa serikali ya Kirumi (Mdo. 28:14–31; Rum. 1:7, 15–16).