Ushindani Ona pia Uasi Mashindano, kubishana, na ugomvi. Ushindani, hususani kati ya waumini wa Kanisa la Bwana au kati ya wana familia, haimpendezi Bwana. Usiwepo ugomvi kati ya mimi na wewe, Mwa. 13:8. Kiburi huleta ushindani, Mit. 13:10. Kama mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake, asamehe kama Kristo alivyowasamehe, Kol. 3:13. Jiepushe na maswali ya kipuuzi na magomvi, Tit. 3:9. Bwana anawaamuru wanadamu wasibishane wao kwa wao, 2 Ne. 26:32. Hamtawaacha watoto wenu wapigane na kuzozana wao kwa wao, Mos. 4:14. Alma aliamuru kwamba pasiwepo na ushindani miongoni mwa waumini wa Kanisa, Mos. 18:21. Shetani alisambaza uvumi na ushindani, Hel. 16:22. Ibilisi ndiye baba wa ushindani na huwachochea wanadamu kubishana wao kwa wao, 3 Ne. 11:29 (Mos. 23:15). Ihubirini injili yangu, ili pasiwepo na ushindani mwingi, M&M 10:62–64. Komeni kubishana ninyi kwa ninyi, M&M 136:23.