Rutu
Katika Agano la Kale, ni mkwe Mmoabu wa Naomi na Elimeleki, waliokuwa Waisraeli. Baada ya kifo cha mume wake, Rutu aliolewa na jamaa ya Naomi, Boazi. Mwana wao Obedi alikuwa babu wa Daudi na Kristo. Hadithi ya Rutu inaelezea kwa uzuri zaidi uongofu wa asiye Mwisraeli katika kundi la kondoo la Israeli. Rutu aliachana na Mungu wake wa zamani na maisha yake ya zamani ili kuungana na jamaa ya waaminio katika kumtumikia Mungu wa Israeli (Rut. 1:16).
Kitabu cha Rutu
Mlango wa 1 unaelezea maisha ya Elimeleki na familia yake katika Moabu. Baada ya vifo vya waume zao, Naomi na Rutu walikwenda Bethlehemu. Mlango 2 unaelezea kwamba Rutu alivuna masazo katika mashamba ya Boazi. Mlango wa 3 unasimulia namna Naomi alivyomwagiza Rutu kwenda katika uga wa kupuria na kulala katika miguu ya Boazi. Mlango wa 4 ni historia ya ndoa ya Rutu na Boazi. Wakazaa mwana, Obedi, ambaye toka ukoo wake Daudi na Kristo wamekuja.