Misaada ya Kujifunza
Ndoa, Oa, Olewa


Ndoa, Oa, Olewa

Agano au mkataba wa kisheria kati ya mwanaume na mwanamke ambalo huwafanya kuwa mume na mke. Ndoa imeamriwa na Mungu (M&M 49:15).

Agano Jipya na la Lisilo na Mwisho la Ndoa

Ndoa iliyofungwa chini ya sheria ya injili na ukuhani mtakatifu ni kwa maisha ya duniani na kwa milele. Wanaume na wanawake wenye kustahili wakiwa wamefungwa hivi hekaluni katika ndoa wanaweza kuendelea kuwa kama mume na mke kwa milele.

Ndoa ya imani mbili

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke wa imani za dini na desturi zilizo tofauti.

Ndoa ya wake wengi

Ndoa ya mume kwa wake wawili au zaidi walio hai. Ni sheria kwa mwanaume kuwa na mke mmoja tu, isipokuwa Bwana anaamuru vinginevyo kwa ufunuo (Yak. [KM] 2:27–30). Kwa ufunuo, ndoa ya wake wengi ilifanyika katika nyakati za Agano la Kale na katika siku za mwanzoni za Kanisa lililorejeshwa kwa maelekezo ya nabii ambaye alishikilia funguo za ukuhani (M&M 132:34–40, 45). Haifanyiki tena katika Kanisa (TR 1); leo, kuwa na zaidi ya mke mmoja kunamzuia mtu kuwa mwanachama katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.