Majivuno, Siofaa Ona pia Kiburi; Malimwengu Uwongo au udanganyifu; kiburi. Siofaa na majivuno yanaweza pia kumaanisha bure au yasiyo na thamani. Mtu asiyeiinua nafsi kwa kiburi atasimama katika mahali patakatifu pa Bwana, Zab. 24:3–4. Wakati mnaposali, msitumie kurudia maneno yasiyofaa, Mt. 6:7. Lile jengo kubwa na lililo pana ni mawazo yasiyofaa na kiburi, 1 Ne. 12:18. Je, mtaendelea kuiweka mioyo yenu juu ya mambo ya ulimwengu yasiyofaa, Alma 5:53. Msiyafuate mambo yasiyofaa ya ulimwengu huu, kwa maana hamwezi kwenda nayo, Alma 39:14. Kiburi na kutoamini vimeleta Kanisa chini ya hukumu, M&M 84:54–55. Wakati tunapojaribu kuridhisha tamaa zetu zisizofaa, mbingu hujitoa, M&M 121:37.