Kosea Kuvunja sheria takatifu, kutenda dhambi, au kusababisha kukosekana kwa faraja, au kujeruhi, pia kuchukiza au kuudhi. Ndugu aliyekosewa ni mgumu zaidi kumpata kuliko mji wenye nguvu, Mit. 18:19. Kama jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe, Mt. 5:29. Yoyote atakayewakosea mmoja wapo wa wadogo hawa waniaminio, ingekuwa heri kuzama baharini, Mt. 18:6 (M&M 121:19–22). Kama kaka au dada yako amekukosea na akakiri, patana naye, M&M 42:88. Katika lolote mwanadamu hamkosei Mungu, isipokuwa wale wasiokiri mkono wake na wasiotii amri zake, M&M 59:21.