Babeli, Babilonia
Mji mkuu wa Babilonia.
Babeli ulianzishwa na Nimrodi na ulikuwa mmoja kati ya miji ya zamani zaidi katika nchi ya Mesopotania, au Shinari (Mwa. 10:8–10). Bwana aliivuruga lugha wakati watu walipokuwa wakijenga Mnara wa Babeli (Mwa. 11:1–9; Eth. 1:3–5, 33–35). Babilonia baadaye ukaja kuwa mji mkuu wa Nebukadneza. Alijenga mji mkubwa kupita kiasi ambao magofu yake bado yapo. Babilonia ukawa mji mwovu sana na toka hapo umekuwa ishara ya uovu wa ulimwengu.