Njia Ona pia Tembea, Tembea na Mungu; Yesu Kristo Mapito au uelekeo ambao mtu huufuata. Yesu alisema ya kuwa Yeye ni njia (Yn. 14:4–6). Uzishike amri za Bwana upate kwenda katika njia zake, Kum. 8:6. Mfundishe mtoto katika njia zimpasazo, Mit. 22:6 (2 Ne. 4:5). Bwana alisema njia zake ni za juu zaidi kuliko njia zetu, Isa. 55:8–9. Mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, Mt. 7:13–14 (3 Ne. 14:13–14; 27:33; M&M 132:22, 25). Mungu atawafanyia njia ili mwepuke majaribu, 1 Kor. 10:13. Bwana hatoi amri ambayo hatayarishi njia kwa ajili ya watoto wake kuishika, 1 Ne. 3:7 (1 Ne. 9:6; 17:3, 13). Hakuna njia nyingine isipokuwa kwa kupitia mlangoni, 2 Ne. 9:41. Mko huru kujiamulia wenyewe—kuchagua njia ya mauti yasiyo na mwisho au uzima wa milele, 2 Ne. 10:23. Hii ndiyo njia na hakuna njia nyingine au jina jingine, 2 Ne. 31:21 (Mos. 3:17; Alma 38:9; Hel. 5:9). Kwa zawadi ya Mwanawe Mungu ametayarisha njia iliyo bora zaidi, Eth. 12:11 (1 Kor. 12:31). Kila mtu alitembea katika njia yake mwenyewe, M&M 1:16. Lazima ifanyike katika njia yangu mwenyewe, M&M 104:16.