Misaada ya Kujifunza
Mosia, Mwana wa Benjamini


Mosia, Mwana wa Benjamini

Mfalme mwaminifu wa Wanefi na nabii katika Kitabu cha Mormoni. Mosia alifuata mfano mwema wa baba yake (Mos. 6:4–7). Alitafsiri mabamba ishirini na manne ya dhahabu yaliyokuwa na kumbukumbu ya Wayaredi (Mos. 28:17).

Kitabu cha Mosia

Kitabu katika Kitabu cha Mormoni. Mlango wa 1–6 ina mahubiri yenye nguvu ya kwa watu wake. Roho wa Bwana akagusa mioyo yao na watu wakaongolewa na hawakusikia tena tamaa ya kutenda maovu. Mlango wa 7–8 husimulia juu ya kikundi cha Wanefi waliokwenda kuishi katika nchi ya Walamani. Kikundi cha watafutaji kilitumwa kwenda kuwatafuta. Ammoni kiongozi wa kikundi cha watafutaji, aliwaona na akajifunza hadithi juu ya majaribu yao chini ya ukandamizaji wa Walamani. Mlango wa 9–24 inaelezea ukandamizaji huo na namna viongozi wao—Zenifa, Nuhu, na Limhi—walivyoishi chini ya Walamani. Kifo cha kishahidi cha nabii aliyeitwa Abinadi pia kimeandikwa. Alma aliongolewa wakati wa kesi ya Abinadi. Mlango wa 25–28 inaelezea hadithi ya namna mwana wa Alma na wana wanne wa Mfalme Mosia walivyokuja kuongolewa. Katika mlango wa 29 mfalme Mosia alipendekeza kwamba utaratibu wa waamuzi utumike badala ya wafalme. Alma mwana wa Alma aliteuliwa mwamuzi mkuu wa kwanza.