Sikio Ona pia Sikiliza Katika maandiko sikio mara nyingi limetumika kama alama ya uwezo wa mtu wa kusikia na kuelewa mambo ya Mungu. Wanayo masikio, lakini hawasikii, Zab. 115:6. Bwana huniamsha sikio langu lipate kusikia, Isa. 50:4–5 (2 Ne. 7:4–5). Mwenye masikio ya kusikia, na asikie, Mt. 11:15. Masikio yao hayasikii, Mt. 13:15 (Musa 6:27). Jicho haliyaoni wala sikio halikuyasikia mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao, 1 Kor. 2:9 (M&M 76:10). Ibilisi anongʼona masikioni mwao, 2 Ne. 28:22. Fungueni masikio yenu ili mpate kusikia, Mos. 2:9 (3 Ne. 11:5). Niliitwa mara nyingi, na sikutaka kusikia, Alma 10:6. Yapeni sikio maneno yangu, Alma 36:1 (Alma 38:1; M&M 58:1). Hakuna sikio ambalo halitasikia, M&M 1:2. Masikio hufunguliwa kwa njia ya unyenyekevu na sala, M&M 136:32.