Moyo Uliovunjika Ona pia Dhabihu; Mnyenyekevu, Unyenyekevu; Moyo; Pole, Upole; Toba, Tubu Kuwa na moyo uliovunjika ni kuwa mwenye kunyenyekea, kupondeka, mwenye kutubu, na mpole—maana yake, ni kuwa msikivu wa mapenzi ya Mungu. Nakaa pamoja na yeye aliye na roho iliyopondeka na kunyenyekea, Isa. 57:15. Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya wale walio na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, 2 Ne. 2:7. Mtatoa dhabihu kwa Bwana ya moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, 3 Ne. 9:20 (M&M 59:8). Wale tu walio na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka wanapokelewa katika ubatizo, Moro. 6:2. Yesu alisulubiwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi kwa moyo uliopondeka, M&M 21:9. Yule aliye na roho iliyopondeka hukubalika, M&M 52:15. Roho Mtakatifu ameahidiwa kwa wale wenye toba, M&M 55:3. Roho wangu amepelekwa ili kuwaangaza walio wanyenyekevu na wenye toba, M&M 136:33.