Tafsiri
Kuelezea maana ya wazo moja lililotolewa katika lugha moja na kuyaweka katika maneno yaliyo sawa sawa katika lugha nyingine (Mos. 8:8–13; M ya I 1:8). Katika maandiko mara nyingi inaelezwa kama kipawa kutoka kwa Mungu (Alma 9:21; M&M 8; 9:7–9). Wakati mwingine yaweza kumaanisha kuboresha au kusahihisha tafsiri iliyoko katika lugha au kurejesha sehemu ya maneno yaliyopotea (M&M 45:60–61). Joseph Smith aliamriwa kufanya tafsiri ya kuongozwa na Mungu katika Biblia ya toleo la Mfalme James (M&M 42:56; 76:15).