Zeno Nabii wa Israeli katika nyakati za Agano la Kale ambaye unabii wake juu ya huduma ya Kristo unapatikana katika Kitabu cha Mormoni pekee. Alitoa unabii wa maziko ya Kristo na siku tatu za giza, 1 Ne. 19:10, 12. Alitabiri kukusanyika kwa Israeli, 1 Ne. 19:16. Yakobo alinukuu fumbo la Zeno la mti wa mzeituni wa kupandwa na wa porini, Yak. (KM) 5. Yakobo aelezea istiari ya Zeno, Yak. (KM) 6:1–10. Alifundisha kuhusu sala na kuabudu, Alma 33:3–11. Alifundisha kwamba ukombozi huja kupitia Mwana, Alma 34:7. Aliuawa kwa sababu ya ushuhuda wake wa ujasiri, Hel. 8:19. Alisema juu ya urejesho wa Walamani, Hel. 15:11. Alitoa ushuhuda juu ya angamizo wakati wa kifo cha Kristo, 3 Ne. 10:15–16.