Ninawi Ona pia Ashuru; Yona Katika Agano la Kale, ni mji mkuu wa Ashuru na kwa zaidi ya miaka mia mbili ulikuwa mji maarufu wa kibiashara katika kingo ya mashariki ya mto Tigri. Ulianguka wakati wa kushuka kwa ufalme wa Ashuru, 606 K.K. Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliishi Ninawi, 2 Fal. 19:36. Yona alitumwa kuhubiri toba kwa mji ule, Yon. 1:1–2 (Yon. 3:1–4). Watu wa Ninawi walitubu, Yon. 3:5–10. Kristo aliitumia Ninawi kama mfano wa toba mbele ya Wayahudi, Mt. 12:41.