Suleimani Ona pia Bath-sheba; Daudi Katika Agano la Kale, ni mwana wa Daudi na Bath-sheba (2 Sam. 12:24). Sulemani kwa wakati fulani alikuwa mfalme wa Israeli. Daudi alimtaja Sulemani kama mfalme, 1 Fal. 1:11–53. Daudi alimwamuru Sulemani kutembea katika njia za Bwana, 1 Fal. 2:1–9. Bwana alimwahidi moyo wa kufahamu, 1 Fal. 3:5–15. Aliwahukumu akina mama wawili na aliweza kumtambua mama halisi wa mtoto huyo, 1 Fal. 3:16–28. Anena kwa methali na nyimbo, 1 Fal. 4:32. Alijenga hekalu, 1 Fal. 6; 7:13–51. Aliliweka wakfu hekalu, 1 Fal. 8. Alitembelewa na malkia wa Sheba, 1 Fal. 10:1–13. Suleimani alioa nje ya Israeli, na hao wake zake wakaugeuza moyo wake kwa kuwaabudu miungu wa uongo, 1 Fal. 11:1–8. Bwana alimkasirikia Sulemani, 1 Fal. 11:9–13. Alikufa, 1 Fal. 11:43. Daudi alitoa unabii juu ya utukufu wa utawala wa Sulemani, Zab. 72. Sulemani alipokea wake wengi na masuria, lakini wengine hawakuwapokea kutoka kwa Bwana, M&M 132:38 (Yak. [KM] 2:24).