Mzee
Neno mzee limetumiwa katika njia tofauti katika Biblia. Katika Agano la Kale mara nyingi limetumiwa kwa watu walio na umri mkubwa katika kabila, ambalo kwa kawaida walikuwa wameaminiwa kwa mambo ya kiutawala (Mwa. 50:7; Yos. 20:4; Rut. 4:2; Mt. 15:2). Umri na uzoefu wao ulifanya ushauri wao kuwa wenye thamani. Nafasi yao haikuwa lazima kwa wito wa ukuhani.
Walikuwepo pia wazee waliotawazwa katika ukuhani wa Melkizedeki katika Agano la Kale (Ku. 24:9–11). Katika Agano Jipya, wazee wametajwa kama ni ofisi ya ukuhani katika kanisa (Yak. [Bib.] 5:14–15). Miongoni mwa Wanefi walikuwepo pia wazee waliotawazwa katika ukuhani (Alma 4:7, 16; Moro. 3:1). Katika kipindi hiki, Joseph Smith na Oliver Cowdery ndiyo walikuwa wazee wa kwanza kutawazwa (M&M 20:2–3).
Mzee sasa ni cheo kilichotolewa kwa wote wanaoshikilia ukuhani wa Melkizedeki. Kwa mfano, wamisionari wanaume wote hujulikana kama wazee. Pia, Mtume ni mzee, na ni sahihi kusema juu ya washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili au Akidi ya Sabini kwa cheo hiki (M&M 20:38; 1 Pet. 5:1). Wajibu wa wazee waliotawazwa katika Kanisa leo umetolewa katika ufunuo katika siku za mwisho (M&M 20:38–45; 42:44; 46:2; 107:12).