Maji ya Uzima Ona pia Yesu Kristo Mfano wa Bwana Yesu Kristo na mafundisho Yake. Kama vile maji yalivyo muhimu kwa kutupa uzima wa kimwili, Mwokozi na mafundisho Yake (maji ya uzima) ni muhimu kwa uzima wa milele. Kwa shangwe mtachota maji kutoka katika visima vya wokovu, Isa. 12:3. Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, Yer. 2:13. Kama mtu yeyote akiona kiu, na aje kwangu, na anywe, Yn. 4:6–15. Kama mtu yeyote akiona kiu, na aje kwangu, na anywe, Yn. 7:37. Fimbo ya chuma iliongoza kwenye chemchemi ya maji ya uzima, 1 Ne. 11:25. Kunyweni maji ya uzima bure, M&M 10:66. Amri zangu zitakuwa kisima cha maji ya uzima, M&M 63:23.