Ufahamu na ushahidi wa kiroho unaotolewa na Roho Mtakatifu. Ushuhuda pia waweza kuwa tamko rasmi au la kisheria juu ya kile ambacho mtu hukiona kama kweli (M&M 102:26 ).
Simameni kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, Mos. 18:9 .
Hapakuwa na njia ya kuwaokoa watu isipokuwa kuwashawishi kwa ushuhuda halisi, Alma 4:19–20 .
Ninavyo vitu vyote kama ushahidi kwamba mambo haya ni ya kweli, Alma 30:41–44 .
Kwani hamtapata ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani yenu, Eth. 12:6 .
Je, sikusema amani akilini mwako? Ushahidi gani mkubwa unaoweza kuupata kuliko ule utokao kwa Mungu, M&M 6:22–23 .
Na sasa, baada ya shuhuda nyingi zilizokwisha kutolewa juu yake, huu ni ushuhuda wa mwisho wa zote ambao tunatoa juu yake, M&M 76:22–24 .
Nimewatuma kwenda kushuhudia na kuonya watu, M&M 88:81–82 .
Mashahidi hawa sasa wamekufa, na ushuhuda wao bado una nguvu, M&M 135:4–5 .
Henoko aliwaona malaika wakitoa ushuhuda juu ya Baba na Mwana, Musa 7:27 .
Ingawa nilichukiwa na kuteswa kwa kusema kwamba nimeona ono, lakini bado ilikuwa kweli, JS—H 1:24–25 .