Sakramenti
Kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, sakramenti humaanisha ibada ya kushiriki mkate na maji katika ukumbusho wa dhabihu ya Kristo ya kulipia dhambi. Mkate uliokatwakatwa huwakilisha mwili wake uliovunjwa, maji huwakilisha damu yake iliyomwagika kwa kulipia dhambi zetu (1 Kor. 11:23–25; M&M 27:2). Waumini wa Kanisa wenye kustahili wanapopokea sakramenti, huahidi kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo, ili daima kumkumbuka Yeye, na kuzishika amri Zake. Kupitia ibada hii, waumini wa Kanisa hufanya upya maagano yao ya ubatizo.
Katika Karamu ya Mwisho, Yesu aliielezea ibada ya Sakramenti wakati alipokuwa Akila pamoja na wale Mitume Kumi na Wawili (Mt. 26:17–28; Lk. 22:1–20).