Rigdon, Sidney
Mwongofu na kiongozi wa Kanisa wa mwanzoni kabisa katika miaka ya 1830 na mwanzoni mwa miaka ya 1840. Sidney Rigdon alitumikia kwa wakati fulani kama Mshauri wa Kwanza kwa Joseph Smith katika Urais wa Kwanza wa Kanisa (M&M 35; 58:50, 57; 63:55–56; 76:11–12, 19–23; 90:6; 93:44; 100:9–11; 124:126). Baadaye alianguka na akatengwa na Kanisa katika Septemba 1844.