Karama Ona pia Kipawa cha Roho Mtakatifu; Vipawa vya Roho Mungu humpa mwanadamu baraka nyingi na karama. Kuna karama nyingi za kiroho, 1 Kor. 12:4–10. Takeni sana karama zilizo bora, 1 Kor. 12:31. Kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka kwa Mungu, Yak. (Bib.) 1:17. Uwezo wa Roho Mtakatifu ni karama ya Mungu, 1 Ne. 10:17. Wale wasemao hakuna karama hawajui injili ya Kristo, Morm. 9:7–8. Kila karama iliyo njema yatoka kwa Kristo, Moro. 10:8–18. Uzima wa milele ndicho kipawa kilicho kikuu kuliko vyote, M&M 14:7 (1 Ne. 15:36). Karama hutolewa kwa wale wenye kumpenda Bwana, M&M 46:8–11. Wote hawana kila karama iliyotolewa kwao, M&M 46:11–29.