Naftali
Ni wa sita kati ya wana kumi na wawili wa Yakobo na ni mtoto wa pili wa Bilha, mjakazi wa Raheli (Mwa. 30:7–8). Naftali alikuwa na wana wanne (1 Nya. 7:13).
Kabila la Naftali
Baraka za Yakobo juu ya Naftali zimeandikwa katika Mwanzo 49:21. Baraka za Musa juu ya kabila hilo zimeandikwa katika Kumbukumbu 33:23.