Yeroboamu Katika Agano la Kale, Yeroboamu alikuwa mfalme wa kwanza wa upande wa kaskazini ya Israeli iliyogawanyika. Alikuwa mshirika wa kabila la Efraimu. Yeroboamu mwovu aliongoza uasi dhidi ya nyumba ya Yuda na familia ya Daudi. Yeroboamu aliweka sanamu kwa ajili ya watu katika Dani na Betheli kuabudu, 1 Fal. 12:28–29. Ahiya alimkemea Yeroboamu, 1 Fal. 14:6–16. Yeroboamu alikumbukwa kwa kuleta dhambi ya kutisha kwa Israeli, 1 Fal. 15:34 (1 Fal. 12:30).