Mapokeo Imani na desturi ambazo hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine (2 The. 2:15). Katika maandiko, Bwana daima huwaonya walio waaminifu kuepuka mapokeo maovu ya wanadamu (Law. 18:30; Mk. 7:6–8; Mos. 1:5; M&M 93:39–40).