Mwanamke, Wanawake Ona pia Dada; Kaka, Ndugu; Mwanadamu, Wanadamu Mtu mzima wa kike, binti wa Mungu. Neno Mwanamke wakati mwingine hutumika katika maandiko kama cheo cha heshima (Yn. 19:26; Alma 19:10). Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke, Mwa. 1:27 (Musa 2:27; 6:9; Ibr. 4:27). Mwanamke mwema kima chake chapita cha marijani, Mit. 31:10–31. Mwanamke ni utukufu wa mwanamume, 1 Kor. 11:7. Walakini si mwanamume pasipo mwanamke, wala mwanamke pasipo mwanaume katika Bwana, 1 Kor. 11:11. Wanawake wanapaswa kujipamba katika mavazi ya kujisitiri, 1 Tim. 2:9–10. Mimi, Bwana Mungu, hufurahia katika usafi wa kimwili wa wanawake, Yak. (KM) 2:28. Dhambi zako zimesamehewa, nawe u mwanamke mteule, M&M 25:3. Wanawake wanayo haki ya kupata matunzo kwa waume zao, M&M 83:2.