Uzima Ona pia Nuru, Nuru ya Kristo; Uzima wa Milele Kuishi kimwili na kiroho kulikowezeshwa kwa uwezo wa Mungu. Nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, Kum. 30:15–20. Utanijulisha njia ya uzima, Zab. 16:11. Aandamaye haki anaona uzima, Mit. 21:21. Mwenye kuuona uhai wake ataupoteza: naye aupotezaye uhai wake kwa ajili yangu, atauona, Mt. 10:39 (Mt. 16:25; Mk. 8:35; Lk. 9:24; 17:33). Mwana wa Mtu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa, Lk. 9:56. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu, Yn. 1:4. Yeye amwaminiye aliyenipeleka amepita kutoka mautini kuingia uzimani, Yn. 5:24. Mimi ni njia, kweli, na uzima, Yn. 14:6. Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini zaidi, 1 Kor. 15:19–22. Uchamungu unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuja baadaye, 1 Tim. 4:8. Watoto wetu wapate kutazamia ule uzima uliomo katika Kristo, 2 Ne. 25:23–27. Maisha haya ndiyo wakati wa wanadamu kujitayarisha kukutana na Mungu, Alma 34:32 (Alma 12:24). Mimi ndimi nuru na uzima wa ulimwengu, 3 Ne. 9:18 (Mos. 16:9; 3 Ne. 11:11; Eth. 4:12). Heri wale walio waaminifu, katika uzima au katika mauti, M&M 50:5. Huu ndiyo uzawa wa milele—kumjua Mungu na Yesu Kristo, M&M 132:24. Hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu, Musa 1:39.