Ufunuo wa Yohana
Kitabu cha mwisho katika Agano Jipya, kilicho na ufunuo uliotolewa kwa Yohana Mtume. Aliruhusiwa kuona historia ya ulimwengu, hususani siku za mwisho (Ufu. 1:1–2; 1 Ne. 14:18–27; M&M 77). Ufunuo wa Yohana pia hujulikana kama Apokalisi.
Yohana alipokea ufunuo katika siku ya Bwana katika kisiwa cha Patmo (Ufu. 1:9–10), ngʼambo ya pwani ya Asia, siyo mbali na Efeso. Tarehe halisi ya ufunuo huu haijulikani.
Funguo za kukielewa kitabu hiki zimejumuishwa katika 1 Nefi 14:18–27 na Mafundisho na Maagano 77 (Eth. 4:15–16).
Mlango wa 1–3 ni utangulizi kwa kitabu hiki na barua kwa makanisa saba katika Asia. Yohana aliandika barua hizi ili kuwasaidia Watakatifu kutatua matatizo fulani. Mlango wa 4–5 imeandikwa maono ambayo Yohana alipokea yenye kuonyesha ukuu wa enzi na uwezo wa haki ya Mungu na Kristo. Katika mlango wa 6–9, 11, Yohana ameandika kuwa aliona kitabu kilichotiwa mihuri saba, kila muhuri unawakilisha miaka elfu moja ya historia ya muda ya dunia. Mlango huu kimsingi hujishughulisha na matukio yaliyomo katika muhuri wa saba (ona Ufu. 8–9; 11:1–15). Mlango wa 10 unaelezea juu ya kitabu ambacho Yohana alikila. Kitabu kinawakilisha huduma ya baadaye ambayo yeye angeifanya. Mlango wa 12 unaandikwa ono la ule uovu ambao ulianzia mbinguni wakati Shetani alipoasi na kutupwa nje. Vita vilivyoanza huko vinaendelea kupiganwa duniani. Katika mlango 13, 17–19, Yohana anaelezea falme ovu za kidunia zinazodhibitiwa na Shetani na akaandika maangamizo yake, ikijumuisha angamizo la mwisho la uovu. Mlango wa 14–16 huelezea uadilifu wa Watakatifu katikati ya uovu muda mfupi kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Mlango wa 20–22 inaelezea juu ya Milenia, mji mzuri wa Yerusalemu Mpya, na matukio ya mwisho ya historia ya dunia.