Ishmaili, Mwana wa Ibrahimu Ona pia Hajiri; Ibrahimu Katika Agano la Kale, ni mwana wa Ibrahimu na Hajiri, Mmisri aliyekuwa mjakazi wa Sara (Mwa. 16:11–16). Bwana aliwaahidi wote Ibrahimu na Hajiri kwamba Ishmaili angelikuwa baba wa taifa kubwa (Mwa. 21:8–21). Agano lilikuja kupitia Isaka na siyo Ishmaeli, Mwa. 17:19–21 (Gal. 4:22–5:1). Mungu alimbariki Ishmaili ili angekuwa mwenye kuzaa, Mwa. 17:20. Ishmaili alisaidia kumzika Ibrahimu, Mwa. 25:8–9. Wana kumi na wawili wa Ishmaili walipewa majina, Mwa. 25:12–16. Ishmaili alikufa, Mwa. 25:17–18. Esau alimchukua binti wa Ishmaili, Mahalati, kuwa mke wake, Mwa. 28:9.