Umoja Ona pia Mungu, Uungu Kuwa wamoja katika mawazo, tamaa, na madhumuni kwanza na Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo, na kisha na Watakatifu wengine. Ni vyema kwa ndugu kukaa katika umoja, Zab. 133:1. Mimi na Baba tu wamoja, Yn. 10:30 (M&M 50:43). Yesu alisali kwamba wote wapate kuwa wamoja kama yeye na Baba yake walivyo wamoja, Yn. 17:11–23 (3 Ne. 19:23). Nawasihi kwamba pasiwe na mgawanyiko miongoni mwenu, bali kwamba muwe mumeungana pamoja kwa ukamilifu, 1 Kor. 1:10. Mdhamirie katika nia moja na katika moyo mmoja, mkiungana katika mambo yote, 2 Ne. 1:21. Watakatifu inapaswa mioyo yao ishonwe pamoja katika umoja, Mos. 18:21. Yesu alisali kwa ajili ya umoja miongoni mwa wanafunzi wake Wanefi, 3 Ne. 19:23. Wanafunzi waliungana katika kusali na kufunga kwa bidii, 3 Ne. 27:1. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni wamoja, M&M 20:27–28 (M&M 35:2; 50:43). Ni wajibu wako kuungana na Kanisa la kweli, M&M 23:7. Lolote mtakaloomba kwa imani, mkiwa mmeungana katika sala, mtapata, M&M 29:6. Kama si wamoja ninyi sio wangu, M&M 38:27. Bwana aliwaita watu wake Sayuni kwa sababu walikuwa wenye moyo mmoja na nia moja, Musa 7:18.