Hekalu, Nyumba ya Bwana
Kwa maana iliyo wazi ni nyumba ya Bwana. Bwana daima amekuwa akiwaamuru watu Wake kujenga mahekalu, majumba matakatifu ambamo ndani yake Watakatifu wenye kustahili wanafanya sherehe na ibada takatifu za injili kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya wafu. Bwana huyatembelea mahekalu Yake, nayo ni matakatifu zaidi ya sehemu nyingine zote za kuabudu.
Hema lililojengwa na Musa na wana wa Israeli lilikuwa ni hekalu linalobebeka. Waisraeli walilitumia wakati wa uhamaji wao kutoka Misri.
Hekalu linalofahamika vizuri zaidi na kutajwa katika Agano la Kale ni lile lililojengwa na Sulemani katika Yerusalemu (2 Nya. 2–5). Liliangamizwa katika mwaka 587 K.K. na Wababilonia na likajengwa upya na Zerubabeli takribani miaka 70 baadaye. (Ezra 1–6). Sehemu ya hekalu hili ilichomwa moto katika mwaka 37 K.K.; na Herode Mkuu baadaye akalijenga tena. Warumi wakaliangamiza hekalu hilo katika mwaka 70 B.K.
Katika Kitabu cha Mormoni, wafuasi waadilifu wa Mungu waliongozwa kujenga na kuabudu katika hekalu (2Â Ne. 5:16; Mos. 1:18; 3Â Ne. 11:1). Kujenga na kutumia hekalu kiusahihi ni ishara za Kanisa la kweli katika kipindi chochote, ikiwa ni pamoja na Kanisa la urejesho katika siku zetu. Hekalu la Kirtland lilikuwa ndiyo hekalu la kwanza kujengwa na kuwekwa wakfu kwa Bwana katika kipindi hiki. Toka wakati huo mahekalu yamekuwa yakiwekwa wakfu katika nchi nyingi kote duniani.