Askofu Ona pia Ukuhani wa Haruni Humaanisha “msimamizi,” ni ofisi au nafasi yenye madaraka. Askofu ni ofisi iliyotawazwa katika Ukuhani wa Haruni (M&M 20:67; 107:87–88), na askofu ni mwamuzi wa wote katika Israeli (M&M 107:72, 74). Roho Mtakatifu amewafanya ninyi kuwa waangalizi, Mdo. 20:28. Sifa za kuwa maaskofu zawekwa, 1 Tim. 3:1–7 (Tit. 1:7). Askofu atatawazwa, M&M 20:67. Edward Partridge atahudumu kama askofu kwa Kanisa, M&M 41:9. Askofu atatambua vipawa vya kiroho, M&M 46:27, 29. Kuhani mkuu anaweza kuzitenda kazi katika ofisi ya askofu, M&M 68:14, 19 (M&M 107:17). Askofu huteuliwa na Bwana, M&M 72. Askofu atawaangalia maskini, M&M 84:112. Askofu atasimamia mambo yote ya kimwili, M&M 107:68. Askofu ndiye rais wa Ukuhani wa Haruni, M&M 107:87–88.