Kuhani, Ukuhani wa Melkizedeki
Mtu anayefanya ibada za kidini kwa ajili ya wengine na huzielekeza kwa Mungu. Mara kwa mara katika maandiko, makuhani kwa kweli ni makuhani wakuu kwa mfano wa Melkizedeki (Alma 13:2). Wale wapokeao utimilifu wa utukufu wa Mungu baada ya Ufufuko huwa makuhani na wafalme katika ulimwengu wa selestia.