Waefeso, Waraka kwa
Katika Agano Jipya ni waraka ulioandikwa na Mtume Paulo kwa Watakatifu wa Efeso. Waraka huu una umuhimu mkubwa, kwani unayo mafundisho ya Paulo juu ya Kanisa la Kristo.
Mlango wa 1 una salamu ya kawaida. Mlango wa 2–3 inaelezea mabadiliko ambayo hutokea ndani ya watu wakati wanapokuwa wanachama wa Kanisa—wanakuwa washirika pamoja na Watakatifu, pamoja na Wayunani na Wayahudi wakiwa wameungana katika Kanisa moja. Mlango wa 4–6 inaelezea nafasi ya Mitume na manabii umuhimu wa umoja, na umuhimu wa kuvaa deraya zote za Mungu.