Amuleki Ona pia Alma, Mwana wa Alma Katika Kitabu cha Mormoni, ni mmisionari mwenza wa Alma, mwana wa Alma. Alitembelewa na malaika, Alma 8:20; 10:7. Alimkaribisha Alma nyumbani mwake, Alma 8:21–27. Alihubiri kwa nguvu kwa watu wa Amoniha, Alma 8:29–32; 10:1–11. Alikuwa wa uzao wa Nefi, Lehi, na Manase, Alma 10:2–3. Alishuhudia juu ya ukweli, Alma 10:4–11. Aliwasihi watu watubu na akakataliwa, Alma 10:12–32. Alipambana na Zezromu, Alma 11:20–40. Alifundisha juu ya ufufuko, hukumu, na urejesho, Alma 11:41–45. Alitaka kukomesha mauaji ya waumini, Alma 14:9–10. Alifungwa gerezani pamoja na Alma, Alma 14:14–23. Alivunja kamba za gereza na kuwa huru kwa njia ya imani, Alma 14:24–29. Alishuhudia juu ya Upatanisho, neema, na haki, Alma 34:8–16. Alifundisha juu ya sala, Alma 34:17–28. Aliwahimiza watu wasiahirishe toba, Alma 34:30–41. Imani ya Alma na Amuleki ilisababisha kuta za gereza kuanguka, Eth. 12:13.