Yeriko Mji uliozungushiwa ukuta katika bonde la Yordani ulio futi 800 (mita 245) chini ya usawa wa bahari. Yeriko uko karibu na mahali ambapo Waisraeli walivuka mto wakati walipoingia kwa mara ya kwanza katika nchi ya ahadi (Yos. 2:1–3; 3:16; 6). Waisraeli walipigana vita hapo Yeriko, Yos. 6:1–20. Yoshua aliweka laana juu ya Yeriko, Yos. 6:26 (1 Fal. 16:34). Yeriko ilikuwa ndani ya himaya iliyopangiwa kwa Benjamini, Yos. 18:11–12, 21. Bwana aliitembelea Yeriko katika safari yake ya mwisho ya Yerusalemu, Mk. 10:46 (Lk. 18:35; 19:1).